28 Machi 2025 - 00:38
Mwaliko (Wito) wa Ayatollah Ramadhani kwa watu wa Gilan Kushiriki Katika Maandamano ya Siku ya Quds ya 2025

Ayatollah "Reza Ramezani", Mwakilishi wa Wananchi wa Gilan katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi, katika Mkesha wa Siku ya Quds Duniani, amewaalika na kuwahimiza watu kushiriki katika Maandamano ya Siku hii.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s) na Mwakilishi wa Wananchi wa Gilan katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi, katika mkesha na mnasaba wa Siku ya Quds Duniani, amewaalika na kuwahimiza watu kushiriki kwa wingi katika Maandamano ya Siku hii.

Nakala kamili ya taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Kutokana na kuongezeka uovu wa utawala haram na ghasibu wa Kizayuni na uungaji mkono wa kidhulma wa Marekani katika jinai na mauaji ya kikatili kwa watu wanaodhulumiwa na wasio na ulinzi na himaya wa Palestina, dhamiri ya kimataifa ya mtazamo wa pande mbili (ndumakuwili) na wa kutojali wa jumuiya ya kimataifa kuhusu ukiukaji wa usitishaji vita na kuendelea kwa mauaji ya halaiki ya utawala huo ghasibu, itapelekea kila siku dunia nzima izidi kuamka na kuwa macho.

Wakati huo huo, mikono mitupu ya watu walio na huzuni na Waislamu wa Palestina inaelekea juu katika anga ya wazi ya Mwezi Mtukufu katika Mwezi huu Mtukkufu wa Ramadhani, ili kwa neema ya Mwenyezi Mungu na kwa msaada wa vikosi vya Mapambano ya Upinzani (Muqawamah)  vya eneo hili la Kikanda na kwa Dua zenu enyi watu wenye kufunga na waumini, muweze kufungua macho yenu (kuwa macho) katika kungojea Mwokozi wa Wadhulumiwa na (kushuhudia) Maangamizi ya watu madhalimu.

Bila shaka, hatua madhubuti na vilio vikali vya watu wa Mwenyezi Mungu wa Gilan katika Barabara za Mji na Vijiji, mtaungana na mwangwi wa Taifa huru la Kiislamu la Iran, ili adui ajutie unyakuzi wa ardhi ya Kiislamu na mauaji yao ya halaiki, na aweze kutambua azma na itikadi yetu ya kufika kwenye ardhi ya Quds Tukufu.

Hakika sisi tupo kwenye Ahadi yetu ewe Quds
Reza Ramezani
Mwakilishi wa watu wa Gilan katika Baraza la Wataalam wa Uongozi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha