Mkutano huo uliangazia masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu, huku viongozi hao wakitoa salamu za rambirambi na kuzungumzia nafasi ya uongozi wa Kiislamu pamoja na umuhimu wa mshikamano wa Waislamu.
Marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika nyanja za kielimu, ikiwemo nafasi yake kama Katibu wa Baraza la Wanazuoni wa Ahlul-Bayt (a.s), na alikuwa miongoni mwa waliotafsiri Qur’an Tukufu kwa lugha ya Kiswahili iliyoitwa Tafsiri Al-Mubin.