14 Juni 2026 - 14:00
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as) Akutana na Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq mjini Baghdad

Mkutano huo uliangazia masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu, huku viongozi hao wakitoa salamu za rambirambi na kuzungumzia nafasi ya uongozi wa Kiislamu pamoja na umuhimu wa mshikamano wa Waislamu.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as), Ayatollah Reza Ramezani, amekutana na Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq, Sheikh Hammam Hamoudi, katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, ambapo viongozi hao walijadili masuala mbalimbali yanayohusu Ulimwengu wa Kiislamu.

Katika mkutano huo, Sheikh Hammam Hamoudi alitoa salamu za rambirambi kufuatia kile alichokitaja kuwa ni kuuawa shahidi kwa Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei, akieleza kuwa tukio hilo ni pigo kubwa na lenye majonzi kwa wapenzi, wafuasi na watetezi wa Wilayah.

Kwa upande wake, Ayatullah Ridha Ramadhani alielezea heshima yake kwa nafasi ya kiongozi huyo, akisema kuwa ushiriki mkubwa wa wananchi kwa zaidi ya siku 100 ni tukio la kipekee lililoimarisha misingi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kuonyesha uungaji mkono usio wa kawaida.

Aidha, alizungumzia sifa alizozitaja kuwa ni za msingi za uongozi wa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, akiwemo uchamungu, elimu ya fiqhi na uadilifu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha