Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Brigedia Yahya Saree, Msemaji wa Jeshi la Yemen, ametangaza katika taarifa yake kuwa kuhusu kutunguliwa na kuharibiwa kabisa kwa ndege isiyo na rubani ya MQ-9 ya Marekani wakati wa operesheni yake dhidi ya jimbo la Marib nchini Yemen.
Ndege hii isiyo na rubani ya MQ-9 ni ya tatu kudunguliwa na walinzi wa anga wa Yemen tangu mwanzoni mwa 2025.
Tangu mwaka 2017, wanajeshi wa Yemen wametungua ndege 20 zisizo na rubani za MQ-9 za Marekani katika anga ya Yemen, ambapo ndege 16 kati ya hizo zilidunguliwa nchini Yemen katika miaka miwili iliyopita.
Jeshi la Marekani hutumia ndege zisizo na rubani za MQ-9 kutekeleza baadhi ya mashambulizi na pia kutambua baadhi ya shabaha muhimu.
Your Comment