Kwa Mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Mratibu JMAT Taifa, na Balozi wa Amani Duniani, Bi. Fatma Fredrick Kikkides ametoa Taarifa kwa Viongozi wa JMAT na Washiriki wa Matembezi ya Hiari ya Amani ya (MHA), na kuwaomba Viongozi wote wa Matembezi ya Hiari na Washiriki wote kuhudhuria katika Mkutano muhimu kuhusiana na jambo hilo utakaofanyika Siku ya Jumatatu, Tarehe 02/06/2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi. Mahali: Ukumbi wa Sheli ya Simba Oil - Mburahati. Taarifa ya Mkutano huo ni kama ifuatavyo:
1. Utangulizi
Ndugu Waheshimiwa Viongozi na Washiriki wa Matembezi ya Hiari ya Amani (MHA), Napenda kuwajulisha kuwa kutakuwa na mkutano muhimu wa viongozi wote wa Matembezi ya Hiari ya Amani kutoka pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Taarifa za Mkutano
-
Tarehe: Jumatatu, 02/06/2025.
-
Muda: Kuanzia saa 2:00 asubuhi.
-
Mahali: Ukumbi wa Sheli ya Simba Oil, Mburahati.
Baada ya Mkutano huu, utafuatiwa na zoezi la upimaji wa afya hadi Siku ya Jumanne, 03/06/2025.
Vigezo vya Umri kwa Washiriki: Kuanzia Miaka 18 hadi 45.
3. Usajili na Mkataba wa Kushiriki
Watakao faulu vipimo vya afya na vetting, pamoja na kuthibitisha utayari wa kushiriki MHA, watajaza fomu maalum za usajili na mkataba wa kufuata sheria na taratibu za Matembezi kwa muda wa siku 20 kuanzia:
Tarehe 19/06/2025 hadi 09/07/2025.
4. Mazoezi Kabla ya Matembezi
Baada ya usajili kukamilika tarehe 03/06/2025, yatafuata mazoezi ya kuimarisha utimamu wa mwili kwa muda wa wiki mbili.
5. Uzinduzi wa Matembezi ya Hiari ya Amani (MHA)
-
Tarehe: Alhamisi, 19/06/2025
-
Muda: Saa 3:00 asubuhi
-
Mahali: Viwanja vya Karimjee.
-
Mgeni Rasmi: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
-
Washiriki wa Uzinduzi wa MHA: Watu 2000.
6. Maelezo ya Matembezi Hayo
-
Idadi ya Washiriki: Watu 300.
-
Umbali: Watatembea kwa umbali wa Km. 452 kwa miguu.
-
Njia: Kutoka Dar -es- Salaam hadi Dodoma.
Lengo kuu la Matembezi haya: Kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu.
Kauli Mbiu:
“Uchaguzi wa AMANI Ndio Msingi wa UTULIVU Wetu.”
7. Salamu za Matembezi
-
#TanzaniaYetuAmaniKwanza
-
#UchaguziWetuAmaniYetu
-
#ChaguaUtulivuDumishaAmani
-
#TwendeDodoma
8. Malengo Madogo ya Matembezi
-
a) Kutangaza fursa za utalii na uwekezaji.
-
b) Kusajili na kutatua migogoro.
-
c) Kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari.
-
d) Kutoa elimu ya fedha na uwekezaji.
-
e) Kufundisha mbinu za kujiajiri kwa vijana.
-
f) Kutangaza maonesho ya biashara.
-
g) Kuhamasisha utamaduni wa asili na michezo.
-
h) Kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.
-
i) Kushuhudia miradi ya maendeleo ya serikali maeneo ya njia.
-
j) Kuzitangaza njia za mawasiliano na uchukuzi katika njia yote ya Matembezi.
9. Kilele cha Matembezi
-
Tarehe: Jumatano, 09/07/2025.
-
Muda: Kuanzia saa 3:00 asubuhi.
-
Mahali: Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center (JKCC), Dodoma.
-
Washiriki: Watu 4,000.
-
Mgeni Rasmi: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Maelfu wa watu wataonyesha heshima yao kwa mashujaa wa Amani waliotembea Km. 452 kwa miguu.
10. Mwongozo Kwa Washiriki
Washiriki wote wanatakiwa kuleta peni na notebook / daftari kwa ajili ya maandalizi na shughuli za Mkutano.
11. Mwisho
Tafadhali unaombwa usikose kuhudhuria. Ikiwa hautopata nafasi, basi tunaomba hakikisha unawajulisha wengine.
UZALENDO NI VITENDO!
Kwa pamoja tunaijenga JMAT na Tanzania Yetu.
Asanteni sana.
BI.FATMA FREDRICK KIKKIDES
Mratibu JMAT Taifa
Balozi wa Amani Duniani.
Your Comment