Fatima

  • Na Mwisho Mwema ni wa Wale Wamchao Mwenyezi Mungu

    Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajiun:

    Na Mwisho Mwema ni wa Wale Wamchao Mwenyezi Mungu

    Marhuma, Ukthti Fatima Mwiru, Miaka yote mpaka mwisho wa Uhai wake, alikuwa mstari wa mbele katika utumishi bora uliotuka wa kuhudumia Uislamu na Waislamu, na alikuwa ni Kinara Mtetezi wa Haki za Wanyonge na Wadhulumiwa wa Palestina, kwa kupaza Sauti yake katika Jamii ya Wanawake na Watu wote katika kuungana na Wanawake na Watoto wa Palestina wanaokumbana na Mauaji ya Kimbari ya Utawala Haram wa Kizayuni.