Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mratibu JMAT-TAIFA na Balozi wa Amani Duniani wa Shirika la Amani la (IWPG), Bi.Fatima Fredrick Kikkides akisalimiana na Mlezi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, Nabii Mkuu Dkt. Geordavie katika Mkutano wa baadhi ya Viongozi wa Jumuiya hii, uliofanyika Jijini Dodoma - Tanzania sambamba na uwepo wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule.
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) inajivunia kuwa na Viongozi imara, wachapa Kazi Usiku na Mchana, wasiojua kuchoka, wenye upendo Mkubwa na Taifa lao la Tanzania, wanaopambania udumishwaji wa Tunu ya Amani na Utulivu wa Taifa letu.
Miongoni wa Viongozi hao shupavu na Tunu ya JMAT-TAIFA ni pamoja na Mratibu JMAT-TAIFA - Bi. Fatima Fredrick Kikkides, kwa hakika Mwanamke huyu ni mtu nusu na ni hazina kwa Taifa letu.
Mkutano huu umekuwa ni miongoni mwa mikutano muhimu (na yenye mafanikioni makubwa) ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) katika harakati zake na majukumu yake ya kudumisha Amani na Utulivu wa Taifa letu la Tanzania na kulitakia Kheri na Baraka Taifa hili kwa ajili ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Wananchi.
Your Comment