Kuhusu Tanzania: Sheikh Dkt. Al-Had Mussa Salum alisisitiza Watanzania kuzingatia funzo la Ghaza na Palestina kwa ujumla: 1-Kulinda amani ni kipaumbele cha juu. 2-Ukosefu wa amani huleta madhila, uharibifu, na umwagaji wa damu. 3-Watanzania wanashauriwa kutatua tofauti zao kwa mazungumzo na makubaliano ili Tanzania iendelee kuwa salama.

2 Desemba 2025 - 20:32

Sheikh Dkt. Al-Had M. Salum Atoa Wito wa Amani:“Tutatue tofauti zetu kwa kukaa katika meza ya mazungumzo, Tuzungumze na Tuilinde Tanzania Yetu”+Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), Sheikh Dkt. Al-Had Mussa Salum, amesisitiza umuhimu wa Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Wapalestina, inayofanyika kila mwaka tarehe 29 Novemba, kuonyesha mshikamano wa wanadunia na kuenzi kumbukumbu ya taifa la Palestina.

Sheikh Dkt. Al-Had M. Salum Atoa Wito wa Amani:“Tutatue tofauti zetu kwa kukaa katika meza ya mazungumzo, Tuzungumze na Tuilinde Tanzania Yetu”+Picha

Mahojiano ya Dkt.Alhad kwa Muhtasari
Sheikh Dkt. Al-Had Mussa Salum alisema:

1_“Siku hii ni muhimu sana kwa wanadunia wote kuonyesha mshikamano wao na Wapalestina kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya taifa lao.”

2_Aliongeza kuwa matukio yanayoendelea Mashariki ya Kati, ikiwemo mauaji ya Wapalestina, wanawake, na watoto wasiokuwa na hatia, ni jambo lisilokubalika kimaadili na kibinadamu.

Sheikh Dkt. Al-Had M. Salum Atoa Wito wa Amani:“Tutatue tofauti zetu kwa kukaa katika meza ya mazungumzo, Tuzungumze na Tuilinde Tanzania Yetu”+Picha

3_Sheikh Al-Had alihimiza taasisi zote za amani na haki za binadamu kuendelea kutetea haki za Wapalestina, kuhakikisha amani Ghaza, na kusimamia utekelezaji wa mapatano ya amani bila kuvunjwa na Israel.

Aidha, alibainisha mchango wa Siku hii ya Kimataifa nchini Tanzania, akisema imewezesha kuonyesha mshikamano na Wapalestina na kuendeleza utamaduni wa amani.

Sheikh Dkt. Al-Had M. Salum Atoa Wito wa Amani:“Tutatue tofauti zetu kwa kukaa katika meza ya mazungumzo, Tuzungumze na Tuilinde Tanzania Yetu”+Picha

Kuhusu Tanzania:
Sheikh Dkt. Al-Had Mussa Salum alisisitiza Watanzania kuzingatia funzo la Ghaza na Palestina kwa ujumla:

1_Kulinda amani ni kipaumbele cha juu.

2_Ukosefu wa amani huleta madhila, uharibifu, na umwagaji wa damu.

3_Watanzania tunapaswa kutatua tofauti zetu kwa mazungumzo na makubaliano ili Tanzania iendelee kuwa salama.

Sheikh Dkt. Al-Had M. Salum Atoa Wito wa Amani:“Tutatue tofauti zetu kwa kukaa katika meza ya mazungumzo, Tuzungumze na Tuilinde Tanzania Yetu”+Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha