Hawza ya Imam Reza (a.s) nchini Tanzania inaendelea kusisitiza katika mipango yake juu ya malezi ya kizazi chenye uelewa, maadili na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

3 Desemba 2025 - 16:54

Chuo cha Dini cha Imam Reza (a.s) nchini Tanzania kimefanya sherehe ya mahafali ya saba ya wahitimu wake +Picha

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Hawza ya Dini ya Imam Reza (a.s) nchini Tanzania imefanya kwa mafanikio makubwa sherehe ya mahafali ya saba ya wahitimu wa kozi yake ya miaka mitatu. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Wanazuoni wa dini, Masheikh, Walimu, Wazazi na wageni waalikwa kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Wakati wa sherehe hiyo, Masheikh na walimu wa Hawza waliwapa wahitimu nasaha mbalimbali, wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza safari ya elimu kwa jitihada, ukweli na uaminifu. Aidha, waliwakumbusha kuwa hatua inayofuata inawaletea jukumu kubwa zaidi, kwani wahitimu hao wanatarajiwa kuendelea na masomo ya kielimu katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa - Kilichopo Jijini Dar-es-Salam - Tanzania.

Chuo cha Dini cha Imam Reza (a.s) nchini Tanzania kimefanya sherehe ya mahafali ya saba ya wahitimu wake +Picha

Mgeni rasmi wa sherehe hiyo alikuwa Hujjatul-Islam Dkt. Ali Taqavi, Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa, ambaye katika salamu zake za pongezi aliwahimiza wahitimu kuendelea kujituma na pia aliwakabidhi zawadi maalum.

Vilevile, Mwl. Sayyid Arif Naqvi, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Hujjatul-Asr Society of Tanzania, katika hotuba yake alikumbusha mambo muhimu kwa wahitimu na wazazi wao. Miongoni mwa mambo aliyosisitiza ni: Ikhlasi katika kutafuta elimu, ushirikiano wa wazazi katika safari ya kielimu ya watoto wao, na umuhimu wa elimu ya dini.

Chuo cha Dini cha Imam Reza (a.s) nchini Tanzania kimefanya sherehe ya mahafali ya saba ya wahitimu wake +Picha

Wahitimu pia walinasihiwa kudumisha subira, juhudi, adabu na ikhlasi katika masomo na maisha yao ya kielimu, ili waweze kuwa mfano mwema katika jamii kwa tabia njema na elimu sahihi ya dini.

Hawza ya Imam Reza (a.s) nchini Tanzania inaendelea kusisitiza katika mipango yake juu ya malezi ya kizazi chenye uelewa, maadili na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Chuo cha Dini cha Imam Reza (a.s) nchini Tanzania kimefanya sherehe ya mahafali ya saba ya wahitimu wake +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha