21 Julai 2025 - 00:16
Katuni ikionyesha "Shambulizi dhidi ya Iran: Jinsi Lilivyoanza na Jinsi Lilivyomalizika!"

Mushikamano na Umoja wa Wananchi wa Taifa la Iran ndio Siri ya Mafanikio na Ushindi Mkubwa dhidi ya Adui wa Iran na Ummah wa Kiislamu kwa ujumla.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tizama Mpangilio huu wa Katuni - Picha tatu zikionyesha: “Jinsi Shambulizi dhidi ya Iran Lilivyoanza” vs “Jinsi Lilivyomalizika kwa kichapo kizito cha Iran dhidi ya adui”.

Katuni ikionyesha "Shambulizi dhidi ya Iran: Jinsi Lilivyoanza na Jinsi Lilivyomalizika!"

Picha ya Kwanza: (Jinsi Lilivyoanza) kwa mbwembwe zote huku nyuma ya adui Israel akiwepo Marekani. Waliamini Wanafanya shambulizi hatari Sana huku wakijisemea: “Tutamaliza hili kwa saa chache tu!” - “Iran hawatajua kilichowapata!”

Picha ya Tatu: (Jinsi Shambulizi la Adui Israel Lilivyomalizika): Walipokea kichapo cha Makombora ya Iran, kiasi kwamba mpaka majenerali wao wa Kijeshi wakachafukwa, wakasambaratishwa, wakatandikwa, Israel ikashuhudia mvua ya Makombora ya Iran, na vifaa vyao vya Kijeshi na Kambi zao zao za Kijeshi na vituo vyao Mbalimbali vya Kijeshi vikageuzwa kuwa majivu.

Marekani nayo ikararuliwa huko katika Kambi yake ya Kijeshi ya Al-Udaida iliyopo Nchini Qatar. Ikabidi Marekani na Israel wainue bendera nyeupe ya kusalimu amri na kuomba Suluhu na Iran ila kusimamisha vita.

 “Mushikamano” na Umoja wa Wananchi wa Taifa la Iran ndio Siri ya Mafanikio na Ushindi Mkubwa dhidi ya Adui wa Iran na Ummah wa Kiislamu kwa ujumla.

Kitu adui hawezi kusahau katika uchokozi wake dhidi ya Iran ni droni za kivita za Iran na Makombora hatari tena ya Kizazi cha zamani yaliyotumika kuitwanga Israel na Washirika wake wakashindwa kupambana na kuyazuia Makombora ya Kizazi cha zamani cha Makombora ya Iram.

Swali ni hili: Ingekuwaje Iran ingeamua kufungua milango ya Kambi zake za Makombora ya Kizazi kipya?!, swali hilo liliifanya Israel kuona ulazima wa kuomba Suluhu na kukiri Iran ni Moto wa kuotea mbali na kwamba walikosea katika hesabu zao.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha