20 Juni 2025 - 19:11
Taarifa kutoka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kuhusu Wimbi la 17 la Mashambulizi Mchanganyiko dhidi ya Utawala wa Kizayuni

Vituo hivi vimekuwa kitovu cha uovu dhidi ya wadhulumiwa wa Gaza, Lebanon, Yemen, na pia katika vita vilivyowekwa kwa uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tangu Kimbunga cha Al-Aqsa kilipoanza.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii Ijumaa (20-06-2025), Jeshi la Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, limefanya Mashambulizi ya Makombora na Droni dhidi ya Utawala Haram wa Kizayuni. Shambuli la Leo ni la wimbi la 17 katika Operesheni yake ya Ahadi ya Kweli 3.

Taarifa kutoka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kuhusu Wimbi la 17 la Mashambulizi Mchanganyiko dhidi ya Utawala wa Kizayuni

Taarifa kamili ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

"Piganeni nao, Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa mikono yenu, atawadhalilisha (maadui hao), na nyinyi (Waumini) atawainueni juu yao(atakupeni nusra juu yao), na atatibu nyoyo za watu wa imani."

Watu wema wa Iran, Awali ya 17 ya Operesheni “Ahadi ya Kweli 3” (Al_Waadu al-Sadiq 3) imetekelezwa kote katika ardhi zinazovamiwa na kukaliwa kimabavu dhidi ya malengo (shabaha) kadhaa, ikijumuisha: Vituo vya kijeshi Kijeshi, viwanda vya ulinzi, vituo vya amri na udhibiti, kampuni zinazosaidia operesheni za kijeshi za serikali ya Kizayuni, na uwanja wa ndege wa Nevatim na Hatzorim.

Vituo hivi vimekuwa kitovu cha uovu dhidi ya wadhulumiwa wa Gaza, Lebanon, Yemen, na pia katika vita vilivyowekwa kwa uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tangu Kimbunga cha Al-Aqsa kilipoanza.

Moto mkubwa na baada ya vituo hivyo kulengwa kwa usahihi katika miji ya Tel Aviv, Haifa, na Be'er Sheva unaonyesha kuwa uwezo wa kushambulia wa Makombora ya Balistiki ya Iran unaendelea kuongezeka zaidi na zaidi hadi adhabu kamili itimie kwa genge la uhalifu la serikali ya kizayuni.

Umoja na kusimama imara kwa watu wa Iran na kwa ujasiri katika Ijumaa ya "Ghadhabu na Ushindi" leo hii, pamoja na ujumbe wenye kutia moyo kutoka kwa wananchi wanaoishi nje ya nchi, msaada wa mataifa huru, vikundi vya upinzani na Marajii Taqlid, kwa ujumla umeimarisha dhamira na ujasiri wa askari wa Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi la Iran, waliopangana na kushikamana kikamilifu katika ulinzi huu mtakatifu.

Taarifa kutoka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kuhusu Wimbi la 17 la Mashambulizi Mchanganyiko dhidi ya Utawala wa Kizayuni

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha