Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Shirika la Kitaifa la Hali za Dharura la utawala wa Kizayuni limetangaza kuwa zaidi ya wananchi 11,000 wa Israel wamelazimika kuyahama makazi yao kufuatia makombora ya Iran.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sehemu kubwa ya waliokimbia bado wako chini ya mshtuko wa kisaikolojia uliosababishwa na mashambulizi hayo. Aidha, kupanda kwa bei ya upangishaji nyumba na malalamiko makubwa dhidi ya utendaji wa serikali ni miongoni mwa changamoto kuu zinazowakabili.
Shirika hilo limekadiria kuwa kurejea kikamilifu kwa wakimbizi hawa majumbani mwao kutachukua miaka kadhaa.
Your Comment