Jenerali Naeini amesema tangu 13 Juni 2025 adui alilenga kuuangusha mfumo wa Kiislamu wa Iran kwa kusababisha machafuko ya kijamii, lakini kwa busara ya Kiongozi Mkuu Sayyid Ali Khamenei (h.a.) na uangalifu wa wananchi, njama hizo zilivunjika. Pia katika ghasia za 8 Januari 2026 na operesheni ya “Ahadi ya Kweli”, juhudi za adui zilikabiliwa na kushindwa kabisa.
Ikinukuu vyanzo vyake vya kijeshi, Redio ya Jeshi la Israel ilithibitisha kurushwa zaidi ya Makombora 50 ya Balistiki kutoka ardhi ya Iran, na ving'ora vya kengele ya hali ya hatari vilisikika katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.