Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jenerali Naeini - Msemaji wa Sepah amesema kwamba: Adui tangu tarehe 13 Juni 2025 alikuwa analenga kuunyang’anya mfumo (Uongozi wa Kiislamu wa Iran) uwezo wa kufanya maamuzi, lakini kwa busara na hekima ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Sayyid Ali Khamenei (Allah Amuhifadhi) mipango yao ilivunjwa mmoja baada ya mwingine.
Lengo la adui lilikuwa kusababisha machafuko ndani ya jamii kwa kutumia shinikizo la maisha, lakini nyoyo za watu zimejikita kwa uongozi wa Kiungu, hivyo njama hii pia ilishindwa.
Katika ghasia za tarehe 8 Januari 2026, huduma za kijasusi za zaidi ya nchi 50 ziliingia uwanjani moja kwa moja na kwa njia zisizo za moja kwa moja.
Lengo kuu lilikuwa ni kuuangusha mfumo wa Kiislamu, lakini uangalifu wa wananchi na nguvu ya dola uliifanya miradi hiyo ishindwe kabisa.
Katika operesheni ya “Ahadi ya Kweli (Al_Wa‘d Al_Sadiq)”, zaidi ya ndege 300 katika nchi za eneo zilijaribu kuzuia makombora yetu, na adui licha ya kutumia mamia ya ndege na mifumo ya ulinzi wa anga, alipatwa na mkanganyiko na kushindwa.
Your Comment