Gazeti la Kiebrania Israel Hayom limeripoti kuwa Saudi Arabia imeomba msaada wa kijasusi kutoka Israel na baadhi ya nchi za eneo hilo, kwa lengo la kuzuia uwezekano wa Mlango wa Bahari wa Bab al-Mandab kuzuiwa na Majeshi ya Yemen.
Jenerali Naeini amesema tangu 13 Juni 2025 adui alilenga kuuangusha mfumo wa Kiislamu wa Iran kwa kusababisha machafuko ya kijamii, lakini kwa busara ya Kiongozi Mkuu Sayyid Ali Khamenei (h.a.) na uangalifu wa wananchi, njama hizo zilivunjika. Pia katika ghasia za 8 Januari 2026 na operesheni ya “Ahadi ya Kweli”, juhudi za adui zilikabiliwa na kushindwa kabisa.
Shirika la Taarifa za Kijeshi la Iraq leo limetangaza kuwa katika operesheni mbalimbali za kiusalama, limefanikiwa kuchukua watu 10 wa kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi, wakiwemo wanawake 2.