Kiongozi Mkuu
-
Sepah: Njama za Adui Kuangusha Mfumo wa Uongozi wa Kiislamu Zashindwa kwa Busara ya Kiongozi Mkuu wa Iran na Uangalifu wa Wananchi
Jenerali Naeini amesema tangu 13 Juni 2025 adui alilenga kuuangusha mfumo wa Kiislamu wa Iran kwa kusababisha machafuko ya kijamii, lakini kwa busara ya Kiongozi Mkuu Sayyid Ali Khamenei (h.a.) na uangalifu wa wananchi, njama hizo zilivunjika. Pia katika ghasia za 8 Januari 2026 na operesheni ya “Ahadi ya Kweli”, juhudi za adui zilikabiliwa na kushindwa kabisa.
-
Jibu la Ayatollah Al-Udhma Sistani Kuhusu Kufuata Maimam wa Sala ya Jamaa Wanaopokea Malipo (Mishahara) za Kiserikali
Ayatollah Al-udhma Al-Sistani, kiongozi mkuu wa Shi’a, katika jibu lake kwa swali kuhusu kufuata maimamu wa sala ya jamaa (imam wa jamaa) wanaopokea haki (ya mishahara) kutoka serikali za Kiislamu, alishauri waumini wasisali nyuma yao, ili nafasi za kidini zilindwe dhidi ya uingiliaji wowote unaowezekana wa serikali.
-
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi: "Taifa la Iran limewashinda Marekani na utawala wa Kizayun;
Wazayuni hawawezi kusababisha majanga yote haya bila msaada wa Marekani. Ujumbe unaodaiwa kutumwa kwa Marekani ni uongo mtupu.”
“Katika vita vya siku 12, taifa la Iran bila shaka liliwashinda Marekani na utawala wa Kizayuni. Wao walikuja kufanya uhalifu na uovu, lakini waliadhibiwa na wakarudi mikono mitupu, bila kufikia malengo yao hata moja - na hilo ni kushindwa kwao kwa hakika.”
-
Mwitikio Mkubwa wa Kauli za Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Duniani: “Kiongozi wa Iran amwambia Trump: Endelea Kuota!”
Ayatollah Khamenei, akimjibu Trump, amesema: “Uliota kuwa umeangamiza nguvu za nyuklia za Iran - basi endelea kuota!”