Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- vyanzo vya kuaminika vimeripoti kuwa, katika kipindi cha miezi michache iliyopita, makundi yanayohusiana na Abu Muhammad al-Joulani yameharibu zaidi ya maeneo 20 ya makaburi na ziarah kwa kutumia vilipuzi, mabomu ya sauti na moto.
Vyanzo hivyo viliiambia Al-Ma’loumah kuwa "taasisi za haki za binadamu zimeyaandikia kumbukumbu mashambulizi haya", na kuongeza: "Misimamo ya kiitikadi yenye misingi ya msimamo mkali inayohubiriwa na baadhi ya wahubiri wa misikiti chini ya udhibiti wa makundi haya, imeanza kuwatia hofu wakazi wa miji, hususan Damascus inayojulikana kwa utofauti wa kidini na kijamii."
Imeelezwa pia kuwa misikiti kadhaa chini ya usimamizi wa wahubiri wanaohusiana na utawala wa al-Joulani sasa imejaa fikra kali za msimamo mkali, hali inayosababisha wasiwasi mkubwa mijini – hususan Damascus ambayo kwa muda mrefu imekuwa mfano wa maelewano kati ya makundi tofauti ya kijamii. Fikra hizi zimekuwa zikisababisha shinikizo la kisaikolojia, hofu na wasiwasi kwa jamii za wachache nchini humo.
Mashambulizi ya vikosi vya al-Joulani dhidi ya makundi ya kidini wachache nchini Syria yameongezeka tangu walipodhibiti sehemu za nchi hiyo, na yamefikia kiwango cha kutia wasiwasi. Miongoni mwa matukio hayo ni mapigano ya umwagaji damu katika mji wa al-Suwayda ulioko kusini mwa Syria, unaokaliwa zaidi na jamii ya Druze, pamoja na mauaji ya halaiki ya Waalawi katika mkoa wa Latakia.
Your Comment