Wakili wa Ikrimah Sabri amesema kwamba mashtaka dhidi yake ni sehemu ya “ufuasi wa kisiasa, kidini na kifikra,” na kwamba mamlaka za Kizayuni haziridhiki na misimamo yake ya kidini na kisiasa na wanajitahidi kunyamazisha sauti yake.
Katika hali ya kuongezeka kwa misimamo mikali nchini Syria, waasi wanaodhibiti Damascus wamechoma moto na kuharibu makaburi na maeneo ya ziarah yanayomilikiwa na makundi ya wachache wa kidini wa Syria.