Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo Ijumaa ya Tarehe: 25 Julai, 2025 sawa na Tarehe: 29 Muharram 1447Hijria, Sala ya Ijumaa imesaliwa katika Madrasa ya Mabinti ya Hazrat Zainab (SA) - iliyopo Kigamboni, Dar-es-Salaam. Imamu wa Sala ya Ijumaa: Samahat Sheikh Dkt.Swaleh Maulid.
Katika tukio hili la ibada na la kijamii, Sala ya Ijumaa ilifanyika kwa ushiriki mkubwa wa wanafunzi wa elimu ya dini wanaosoma Katika Madrasa hii.
Katika khutba yake, Sheikh Dkt. Swaleh alielezea changamoto za kijamii zinazotokana na kuachana na mafundisho ya dini.
Akinukuliwa alisema:
“Maisha ya familia nyingi katika zama hizi yamejengwa juu ya fikra potofu, ambazo chanzo chake kikuu ni ukosefu wa dini na maadili ya kiroho.”
Aidha aliongeza kuwa:
“Njia pekee ya kurejesha utulivu na maadili ndani ya familia ni kurejea kwenye dini, kufahamu kwa undani Qur'an Tukufu na kuishi kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s).”
Sala ilisaliwa kwa nidhamu kubwa na utulivu wa hali ya kiroho, na iliacha athari kubwa kwa washiriki wote katika ibada hii.
Your Comment