sala ya ijumaa
-
Ibada ya Sala ya Ijumaa Yaadhimishwa na Kuhuishwa katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni - Dar-es-Salam
Ibada ya Sala ya Ijumaa ya wiki hii ilifanyika katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni, Dar es Salaam, ikiongozwa na Hujjatul-Islam Sheikh Ghawthi Nyambwa, ambaye katika Khutba zake alizungumzia masuala muhimu ya maisha ya kila siku pamoja na matukio ya mwezi wa Rabiul-Awwal, akisisitiza maisha, haiba na nafasi ya kijamii na kisiasa ya Hazrat Zainab (sa).
-
Sala ya Ijumaa Yaadhimishwa katika Hawza Imam Ridha (as), Ikwiriri
Sala ya Ijumaa ya tarehe 25 Septemba 2026 imefanyika katika Hawza Imam Ridha (as), Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, ikishirikisha wanafunzi, walimu na waumini wanawake na wanaume. Khutba imeangazia fadhila za siku ya Ijumaa, umuhimu wa Sala ya Ijumaa, kujenga uhusiano na Mwenyezi Mungu, kuhuisha imani na kuimarisha umoja wa Kiislamu.
-
Sheikh Swaleh Abdur-Rahman Aeleza Wasia wa Imam Ali (as) Kuhusu Mambo Matano Muhimu Katika Maisha
Sheikh Swaleh Abdur-Rahman, katika Khutba ya Swala ya Ijumaa ya Jamiat Al-Mustafa – Tanzania, ameeleza wasia wa Imam Ali (as) unaosisitiza kumtegemea Mwenyezi Mungu, kumuogopa mtu dhambi yake, kusema “sijui” pale asipojua, kujifunza na kuwa na subira.
-
Malawi: Sheikh Abdulrahman Kachere Aeleza Mafunzo ya Sura ya Az-Zalzalah Katika Khutba ya Ijumaa
Sheikh Abdulrahman Kachere ameeleza mafundisho muhimu yanayopatikana katika Sura Tukufu ya Az-Zalzalah, akisisitiza umuhimu wa kukumbuka Siku ya Kiyama na kuwajibika kwa kila tendo linalofanywa na mwanadamu.
-
Mhadhiri wa Sala ya Ijumaa Tehran: Makombora na Diplomasia Vimeimarisha Mizani ya Nguvu kwa Manufaa ya Iran
Mhadhiri / Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema uwezo wa makombora ya Iran pamoja na diplomasia madhubuti ndivyo vilivyoimarisha mizani ya nguvu kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda mshikamano wa kitaifa na kuimarisha imani ya wananchi.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Makubaliano kati ya Iran na Marekani Yanategemea Kanuni ya “Ahadi kwa Ahadi”
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa makubaliano ya maelewano kati ya Iran na Marekani hayajajengwa juu ya msingi wa kuamini serikali ya Marekani, bali yanazingatia kanuni ya “utekelezaji wa ahadi kwa pande zote,” huku akisisitiza kuwa Iran haitaruhusu Marekani kuingilia masuala ya Mlango wa Hormuz.
-
Khatibu wa Ijumaa Tehran Aonya Marekani na Israel: Mkivuka Mipaka Mtajibiwa kwa Nguvu
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema Rais Donald Trump na Benjamin Netanyahu watakabiliwa na jibu kali na la uthabiti iwapo wataendelea na uchokozi dhidi ya Iran.
-
Imam wa Sala ya Ijumaa wa Baghdad:
"Chanzo cha dosari katika mchakato wa kisiasa wa Iraq ni kutanguliza maslahi binafsi na kujisalimisha kwa mashinikizo ya nje"
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad: Chanzo cha dosari katika mchakato wa kisiasa wa Iraq ni kutanguliza maslahi binafsi na kujisalimisha kwa shinikizo za nje
-
Nakuru - Kenya | Khatibu wa Sala ya Ijumaa Sheikh Abdul Ghani Khatibu Aeleza Siri ya Utukufu wa Bibi Fatima (sa) kupitia Hadithi Tukufu za Mtume(saww)
Sheikh Abdul Ghani aliweka wazi kuwa mapenzi ya Mtume (saww) kwa Bibi Fatima (sa) hayawezi kuchukuliwa kwa mtazamo wa kawaida wa mapenzi ya baba kwa binti yake. Badala yake, ni tamko la kiungu na kijamii linalobainisha nafasi yake adhimu katika Uislamu.
-
Malawi | Sala ya Ijumaa yajadili kuhusu Moto wa Jahannam na Sifa Zake + Picha
Katika maelezo yaliyojaa mazingatio, khatibu alibainisha kuwa Moto wa Jahannamu una mawe yanayochoma hadi kufikia ubongo wa waliomo ndani yake, na kwamba kila aina ya moto ni adhabu maalumu kwa aina fulani ya dhambi, kama zilivyobainishwa katika Hadithi za Mtume.
-
Taqwa na Umuhimu Wake | Ijumaa - Khutba na Sala ya Dhuhri katika Chuo cha Dini cha Wanafunzi wa Kike cha Hazrat Zainab (SA)- Kigamboni - Dar-es-salaam
Lengo Kuu la mada iliyowasilishwa ni: Kukuza roho ya ibada, kuimarisha umoja wa kijamii, na kuhimiza utamaduni wa Sala ya Ijumaa miongoni mwa wanafunzi wa dini
-
Mwaka mmoja tangu marufuku ya kusali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Sadiq(as); Sera iliyoratibiwa mahsusi kulenga Ibada za Kidini nchin Bahrain
Kwa mujibu wa wachambuzi, kulengwa kwa mimbari ya Sala ya Ijumaa si suala la ndani tu, bali ni ishara ya juhudi za serikali ya Bahrain kudumisha uhusiano wa karibu na Israel - hata kama ni kwa gharama ya kukandamiza sauti za kidini na za wananchi.