29 Julai 2025 - 15:47
Madrasa Hazrat Zainab (sa) | Dini na Afya: Dkt. Beshteri Azungumzia Umuhimu wa Lishe Sahihi kwa Muislamu

Dkt. Beshteri alieleza kuhusu adabu za kula chakula kulingana na mafundisho ya Imam Ja’far Sadiq (a.s), akitaja riwaya mbalimbali zinazoelekeza namna bora ya kula kwa mujibu wa maadili ya Kiislamu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Siku ya Jumanne tarehe 29 Julai 2025, kikao maalumu cha kielimu kiliandaliwa katika Madrasa ya Mabinti ya Hazrat Zainab (SA) - iliyopo Kigamboni, Dar-es-salaam -  kwa muda wa dakika 45, kikisimamiwa na Dkt. Mi'mari Beshtari kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Madrasa Hazrat Zainab (sa) | Dini na Afya: Dkt. Beshteri Azungumzia Umuhimu wa Lishe Sahihi kwa Muislamu

Katika kikao hicho, Dkt. Beshteri alitoa mada yenye maudhui hii: “Lishe katika Uislamu”, ambapo alizungumzia kwa kina mambo muhimu yafuatayo:

1_Aina ya vyakula salama (vyenye afya) na athari zake chanya kwa mwili na roho ya Mwanadamu.

2_Madhara ya vyakula visivyo salama (vyenye madhara) na namna vinavyoathiri afya.

3_Wakati muafaka wa kula chakula, kwa mujibu wa Elimu na Mafundisho ya Dini Tukufu ya Kiislamu.

Aidha, Dkt. Beshteri alieleza kuhusu adabu za kula chakula kulingana na mafundisho ya Imam Ja’far Sadiq (a.s), akitaja riwaya mbalimbali zinazoelekeza namna bora ya kula kwa mujibu wa maadili ya Kiislamu.

Kikao hiki kilipokelewa kwa hamasa kubwa na wanafunzi wa kike na kilifanyika katika mazingira ya kielimu na kiroho.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha