Wanafunzi wa Chuo cha Al-Mustafa (s.a.w.w) Mbezi Beach, Dar es Salaam, Tanzania washiriki katika programu ya kiroho ya Dua ya Tawassul, kwa lengo la kuimarisha uhusiano wao na Mwenyezi Mungu na kuendeleza utamaduni wa dua na Tawassul.
Darsa ya maarifa ya Qur’an Tukufu imeendelea kwa wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa – Mbezi Beach, Dar-es-Salaam, katika programu ya kila wiki inayolenga kuwajengea wanafunzi uelewa wa kina kuhusu tafsiri, ujumbe na mafundisho ya Qur’an Tukufu, pamoja na kuwawezesha kuyahusianisha mafundisho hayo na maisha yao ya kila siku.