Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Jamiat Al-Mustafa, Dar -es- Salaam - Tanzania, Chini ya Usimamizi na Uongozi wa Hojjat Al-Islam wal - Muslimin, Dr. Ali Taqavi, inaendesha Kozi muhimu ya Kompyuta kwa Vitendo ya ICDL kwa Wanafunzi (Mabanati) wa Hawzat Sayyidat Zainab (s.a). Kozi hii inayoboresha ujuzi wa ICDL ni moja ya harakati muhimu za Kielimu na Maarifa kwa Mabanati wa Kiislamu wanaosoma katika Hawzat hii.
ICDL inawakilisha Leseni ya Kimataifa ya Fani ya (Computer) Kompyuta. Na hiyo ndio maana ya Kozi hii ya ICDL - Yaani: International Computer Driving License. Hii ni Kozi muhimu katika Kozi za Kompyuta ambazo zinauwezo wa kumsaidia na kumsapoti mtu yeyote kujikwamua Kiuchumi.
Kwa maana kwamba Mwanafunzi atakaposoma Kozi hii, maana yake anakuwa amejipatia Cheti kinachongoza Duniani cha Ujuzi wa Kompyuta.
Wanafunzi hawa wa Hawzat Zahra (sa) wanasoma Kozi hii ya Kompyuta katika kiwango cha Kimataifa kwa ajili ya kufikia hatua ya kujiimarisha zaidi na kuwa na ujuzi wa Ulimwengu wa kidijitali.
Hii ni sehemu moja wapo ya ya zile Harakati za Kielimu na Maarifa zinazoongozwa na kusimamiwa na Hojjatul Islam Dr.Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al_Mustafa (S) - Dar-es-salaam, Tanzania.
Your Comment