Tunawapongeza waalimu waliowafundisha wasichana hawa wa Kiislamu kwa bidii na uaminifu, na pia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Jamiatul Mustafa (s) - Tanzania, Hojjatul Wal Muslimin, Dr.Ali Taqavi aliyekuja na wazo hili muhimu na kulisimamia kwa hekima na juhudi kubwa.
ICDL inawakilisha Leseni ya Kimataifa ya Fani ya (Computer) Kompyuta. Na hiyo ndio maana ya Kozi hii ya ICDL - Yaani: International Computer Driving License. Hii ni Kozi muhimu katika Kozi za Kompyuta ambazo zinauwezo wa kumsaidia na kumsapoti mtu yeyote kujikwamua Kiuchumi.