23 Juni 2025 - 17:34
Imamu wa Ijumaa wa Baghdad: Waislamu wote wanapaswa kusimama na Ayatollah Khamenei

Imamu wa Ijumaa wa Baghdad ametoa taarifa yenye maneno makali kufuatia jinai ya hovyo ya Trump.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (AS) - ABNA - Ayatollah Sayyed Yassin Mousavi, Imam wa Swala ya Ijumaa ya Baghdad, alitoa taarifa yenye maneno makali kufuatia kauli ya mhalifu Trump na yenye kutia chumvi.

Nakala ya kauli yake ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: «إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِی الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِیَعًا» “Hakika Firauni amevuka mipaka (amejivuna mno) katika ardhi na akawafanya watu wake makundi makundi.” (Al-Qasas 4).

Trump ameasi na kufanya uovu na utwaghuti mkubwa katika ardhi, na waoga kama watawala wa nchi za Magharibi na Kiarabu wamemsaidia katika njia hii, ingawa amewaona kuwa ni wanyonge na kuwafedhehesha, na hajapata ujasiri, ushujaa, uthabiti, au heshima ndani yao. Qur’an inawaeleza kama ifuatavyo: «وَضُرِبَت عَلَیهِمُ الذِّلَّةُ وَالمَسکَنَةُ وَباءوا بِغَضَبٍ مِنَ اللَّهِ» “Muhuri wa unyonge na uhitaji uligongwa kwenye vipaji vya nyuso zao, na wakashikwa tena katika ghadhabu ya Mungu.” (Al-Baqarah 61).

Maovu yake na kiburi chake kimeongezeka kwa sababu hakuna mtu aliyesimama dhidi yake, na kwa tuhuma za uwongo, amethubutu kumtishia mtu mwema na mtakatifu na msafi kabisa wa kidini na ambaye ni ngome ya mamlaka, na amefikiria kwamba anaweza kunyoosha mkono wake mchafu kwa Imam Sayyid Ali Khamenei (roho yangu iwe fidia kwake).

Ewe Firauni wa Zama hizi! Je, hujui kwamba vita hivi ni burudani ya vita vya kihistoria vya zamani? Mwenyezi Mungu anasema: 

«وَقَالَ فِرْعَوْنُ ذَرُونِی أَقْتُلْ مُوسَیٰ وَلْیَدْعُ رَبَّهُ ۖ إِنِّی أَخَافُ أَنْ یُبَدِّلَ دِینَکُمْ أَوْ أَنْ یُظْهِرَ فِی الْأَرْضِ الْفَسَادَ (۲۶) وَقَالَ مُوسَیٰ إِنِّی عُذْتُ بِرَبِّی وَرَبِّکُمْ مِنْ کُلِّ مُتَکَبِّرٍ لَا یُؤْمِنُ بِیَوْمِ الْحِسَابِ».

Na Firauni akasema: "Niacheni nimuue Musa, naye amuombe Mola wake Mlezi. Hakika mimi nachelea asikubadilishieni dini yenu au atafanya ufisadi katika nchi." (26).

Yeyote ambaye Mungu yuko pamoja naye hakika ni mshindi.

Hata hivyo, ninawalingania walinzi wote wa dini na watoto wa Kiislamu Mashariki na Magharibi mwa ardhi, hususan Seminari (Hawza) na Mamlaka kubwa za Marajii Taqlid (Dua zao ziendelee), na kauli zao ziendelee katika kulaani kitendo hiki cha aibu kisichoweza kunyamaziwa au kusamehewa.

Umma wa Kiislamu lazima utangaze mshikamano wake na Jamhuri ya Kiislamu katika vita hivi vitakatifu vilivyolazimishwa kwa Iran kupitia Wanajeshi wa Vita vya Misalaba, Wakristo wa Kizayuni na Mayahudi.

Na kila mtu anapaswa kuuhamasisha Umma wa Kiislamu katika vyombo vya habari na nyanja za kiroho kwa kutumia uwezo wao, kutumia nafasi ya mtandaoni, na kufanya mikusanyiko ya kitamaduni yenye utambuzi. Jueni kwamba ushindi aliotuahidi Mwenyezi Mungu uko karibu sana, «وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ الْعَزِیزِ الْحَکِیمِ» “Na ushindi hautokani ispokuwa na Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye Hikima! (Aal Imran 126).

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha