"Msanii mashuhuri na maarufu, Bwana Mahmoud Farshchian, alikuwa nyota angavu katika anga ya sanaa ya Kiirani. Uaminifu wake na ucha Mungu wake vilimuwezesha kuutumia uwezo wake wa kipekee katika kuhudumia maarifa na mambo ya kidini, na ameacha nyuma kazi za sanaa zisizofutika. Rehema na radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Nawasilisha rambirambi za dhati kwa familia yake, marafiki zake, wanafunzi wake, na jamii ya wasanii nchini."