Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, msemaji huyo leo Jumapili, akijibu tangazo la nchi hizo tatu kuhusu kutambua Palestina, alisisitiza kuwa uamuzi huo ni hatua chanya na ya kuunga mkono juhudi za kimataifa kwa ajili ya amani ya Mashariki ya Kati.
21 Septemba 2025 - 20:00
News ID: 1729557

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika taarifa yake amesema kuwa hatua ya kutambua rasmi Taifa la Palestina iliyochukuliwa na Uingereza, Kanada na Australia ni jambo muhimu na la kimaendeleo, kama sehemu ya suluhisho linalojulikana kama mpango wa mataifa mawili.
Your Comment