Maelfu ya wananchi mjini Mexico City waliungana katika maandamano makubwa yaliyopewa jina “Mexico kwa Palestina”, wakilaani jinai za utawala wa Kizayuni na uungaji mkono wa Marekani, huku wakidai kusitishwa kwa mauaji ya kimbari Gaza na kutumwa haraka kwa misaada ya kibinadamu.
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza leo Jumapili kuwa, kutokana na vita na kuzidi kwa mzingiro unaoendelea wa jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza, Wapalestina 1,500 wamepoteza uwezo wao wa kuona.