11 Mei 2025 - 16:05
"Vita vya Gaza vimesababisha Wapalestina 1,500 kupoteza uwezo wa kuona"

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza leo Jumapili kuwa, kutokana na vita na kuzidi kwa mzingiro unaoendelea wa jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza, Wapalestina 1,500 wamepoteza uwezo wao wa kuona.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (as) - ABNA -:  Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza imetangaza kuwa: kutokana na vita vinavyoendelea vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza pamoja na uhaba mkubwa wa dawa, raia wa Palestina wapatao 1,500 wamepoteza uwezo wao wa kuona, huku wengine 4,000 wakikabiliwa na hatari hiyo hiyo.

Mwandishi wa Al Jazeera pia ameripoti kuwa: kufuatia mashambulizi ya leo Jumapili dhidi ya mahema ya wakimbizi katika Mji wa Khan Yunis kusini mwa Gaza, watu 9 wameuawa shahidi, wakiwemo watoto 4.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) nalo limeripoti leo Jumapili kuwa: linayo maelfu ya malori yaliyo tayari kuingia Gaza, na timu zake ziko tayari kupanua shughuli za kusambaza misaada.

Shirika hilo limeongeza kuwa: ikiwa mzingiro kamili wa Gaza ambao umeendelea kwa siku 71 tangu uanze hautakomeshwa, madhara na mateso kwa raia yatazidi kuongezeka.

Aidha, taasisi za haki za binadamu zimeripoti kuwa wazee 14 wa Kipalestina wamefariki dunia wiki iliyopita kutokana na njaa, utapiamlo, na ukosefu wa huduma za afya, hali inayochangiwa na mzingiro mkali wa eneo hilo.

Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Ulaya-Mediterranea kimeripoti kuwa: wazee na watoto wa Kipalestina wanakufa polepole kutokana na hali mbaya ya maisha inayosababishwa kwa makusudi na Israel.

Kuanzia tarehe 18 Machi 2025 hadi sasa, idadi ya mashahidi waliothibitishwa Gaza imefikia 2,710, huku idadi ya majeruhi ikiwa 7,432.

Katika taarifa ya Wizara ya Afya ya Palestina pia imethibitishwa kuwa: tangu kuanza kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza mnamo tarehe 7 Oktoba 2023 (15 Mehr 1402), jumla ya mashahidi imefikia 52,810, na idadi ya majeruhi ni 119,473.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha