Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (A.S) - ABNA - Wanazuoni wa Bahrain, kwa kauli kali na ya wazi, sambamba na kulaani uchokozi wa kikatili wa utawala wa Kizayuni huko Ghaza, wameeleza masikitiko yao juu ya kimya cha jumuiya ya kimataifa na kutokuwa na msaada wa nchi za Kiarabu na Kiislamu mbele ya jinai hizo.
Wanachuoni hawa walisifu subira na ustahimilivu wa watu wa Palestina na kuiona kuwa ni mfano hai wa Jihadi ya Haki dhidi ya batili.
Taarifa hiyo inasema: Uchokozi wa kikatili wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza unaendelea; Mauaji hayo ni ya kuendelea na ya kutisha, na idadi ya wafia dini (Mashahidi) inaongezeka kila siku. Uhalifu huu ni kutozingatia wazi utakatifu wa maisha ya Mwanadamu na ukiukaji wa sheria, mikataba na makubaliano yote ya kimataifa. Wakati huo huo, walimwengu na taasisi zake zote zimetumbukia katika kimya cha kutisha, na Marekani na ulimwengu wa Magharibi zinaendelea kuunga mkono utawala haram wa Kizayuni unaoukalia kwa mabavu Palestina.
Nchi za Kiarabu na Kiislamu pia zimenaswa katika ukimya wa ajabu na wa kutatanisha. Na ni kana kwamba lugha ya watu wa Ghaza inasema: "حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَکِیلُ" / “Mwenyezi Mungu anatutosha, na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa".
Kwa upande mwingine wa hadithi hii, uimara, uthabiti, na upinzani wa watu wa Gaza ni jambo la dhahiri. Watu wanaokataa kujisalimisha na kutokubali kudhulumiwa na kukaliwa kimabavu, na leo hii, wameonyesha mfano hai wa vita vitakatifu kati ya haki na batili; Vita ambayo kushindwa hakuna maana yoyote (vita ambayo haielewi wala kukubali kushindwa kwa sababu haki haishindwi na batili).
Huku tukilaani uchokozi huu wa kikatili na mauaji ya kutisha, pia tunalaani vikali ukimya wa aibu na udhaifu wa baadhi ya Serikali. Wakati huo huo, tunasifu uthabiti na upinzani wa watu wa heshima na wapendwa wa Gaza na tunamwomba Mwenyezi Mungu kwa ufunguzi na ushindi wao dhidi ya maadui zao.
Your Comment