Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna -Ayatollah Al-Udhma Hossein Nouri Hamedani ambaye ni miongoni mwa Marajii Taqlid (wa Madhehebu ya Shia), ametoa ujumbe wa kulaani jinai za hivi karibuni zilizofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni katika nchi za Yemen, Syria na Ukanda wa Ghaza.
Nakala ya ujumbe huu ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Kwa mara nyingine tena utawala huu katili na haramu wa Kizayuni umefanya jinai kubwa na kuwaua kwa umati Wanawake, Wanaume na Watoto katika Ukanda wa Ghaza.
Uhalifu huu unaotia uchungu unafanywa wakati ambao Rais mhalifu wa Amerika alikuwa tayari ameahidi amani.
Hivi leo utawala wa Kizayuni unaoua watoto umeonyesha kwa mara nyingine tena kwamba haufuatilii ahadi zozote na unavunja ahadi (mapatano na maafikiano) kirahisi, na kitendo hicho cha kinyama ndio msingi wa kuangamizwa kikamilifu Taifa Madhulumu la Palestina.
Kutokuwa na dhamira hii ni somo kwa kila mtu kujua kwamba wenye kiburi (waistikbari) hawatafikiria chochote isipokuwa maslahi yao wenyewe na kwa njia hii hawataacha jinai yoyote ile, na (hali ni kama vile) tunavyoona kwamba, kupitia kuwafundisha magaidi na kubadili sura za magaidi, watawaua pia watu wanaodhulumiwa wa Taifa la Syria, na bila ya kutilia maanani, Marekani na washirika wake wanawashambulia watu wanaodhulumiwa wa Taifa la Yemen, na wakati huo huo taasisi na vituo vya kimataifa na wadai bandia wa haki za binadamu wamechukua ukimya wa kutisha na hawajibu mauaji hayo ya kimbari huko Yemen, Syria na Ghaza.
Huku tukilaani uhalifu huu mbaya, tunaomba mataifa yote huru yasizuie msaada wowote wa kimwili na wa kiroho na kutangaza uungaji mkono wao kwa mataifa haya yanayokandamizwa.
Qom Al-Muqaddasa
Hossein Nouri Hamedani
Your Comment