Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as)-ABNA-, mradi wa “Ushonaji kwa ajili ya Palestina” ulianza asubuhi ya jana keshokutwa kwa kuendesha warsha ya kwanza katika Msikiti wa jiji la Cape Town, Afrika Kusini. Katika warsha hiyo, washiriki walishona vipande vya kitambaa vya ukubwa wa sentimita 15 kwa 15 kwa rangi za bendera ya Palestina.

Kila kipande cha kitambaa kinawakilisha kifo cha watoto 10 wa Palestina katika mauaji ya kimbari yanayoendelea Ghaza. Lengo la waandaji ni kushona vipande 2,000 kuashiria kumbukumbu ya zaidi ya watoto 20,000 waliopoteza maisha katika vita hii.

Kulingana na viongozi wa mradi, blanketi itakayoundwa kwa kushona vipande hivyo pamoja, itafunguliwa rasmi siku ya Kimataifa ya Umoja na Watu wa Palestina mnamo tarehe 29 Novemba 2025. Hatua hii ya ishara ni juhudi za pamoja za kuenzi mateso ya watoto wa Ghaza na kuimarisha sauti ya mshikamano wa wananchi wa Cape Town na Palestina.



Your Comment