Hezbollah imetoa tamko likisema kuwa: "Uhalifu na mashambulizi yanayofanywa na wavamizi (yaani utawala wa Kizayuni wa Israel) dhidi ya Yemen ni ishara ya wazi ya kufilisika kwao kisiasa, kiakhlaqi na kijeshi."
Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahrain amesema: A'"shura inatolewa kila mwaka katika vyombo vya habari vya Bahrain kama ishara ya uhuru na uvumilivu wa kidini, lakini kivitendo wafuasi wa Kishia wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na vikwazo vikali, kuanzia kukamatwa na kuandikiwa wito hadi kuharibiwa maeneo ya kidini na mashinikizo ya kubadili mavazi ya kidini.
Katika mkutano na Spika na wabunge wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Iran Haijawahi Kuyumba Mbele ya Mashinikizo ya Kimataifa".