Wachambuzi wa kimataifa wanasema kuwa hatua hii inaongeza mvutano kati ya Tehran na Washington, huku ikionyesha hatari zinazoongezeka kwa usalama wa usafirishaji wa baharini.
Baadhi ya wanaharakati na wafuasi wa Palestina nchini Afrika Kusini wanashona vipande vya kitambaa vyenye rangi za bendera ya Palestina, kuunda kazi ya ishara ya kumbukumbu kwa watoto waliopoteza maisha katika vita vya Ghaza. Kazi hii itafunguliwa rasmi mnamo tarehe 29 Novemba, Siku ya Kimataifa ya Umoja na Palestina.