Kwa mujibu wa Bloomberg, Waziri Mkuu wa Canada alikumbusha kuwa nchi wanachama wa G20 zinajumuisha jumla ya asilimia 75 ya idadi ya watu duniani, sehemu mbili za tatu ya Pato la Taifa la Dunia (GDP) na asilimia 75 ya biashara ya kimataifa.
Baadhi ya wanaharakati na wafuasi wa Palestina nchini Afrika Kusini wanashona vipande vya kitambaa vyenye rangi za bendera ya Palestina, kuunda kazi ya ishara ya kumbukumbu kwa watoto waliopoteza maisha katika vita vya Ghaza. Kazi hii itafunguliwa rasmi mnamo tarehe 29 Novemba, Siku ya Kimataifa ya Umoja na Palestina.
Amesisitiza kuwa: Serikali na wananchi wa Afrika Kusini wanalaani vitendo vya kinyama vya utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya wananchi wa eneo la kikanda hususan watu wa Palestina, Lebanon na Iran.