24 Novemba 2025 - 21:03
Canada: Dunia huko Johannesburg Imeonyesha kuwa Inaweza Kuendelea Hata Bila Marekani

Kwa mujibu wa Bloomberg, Waziri Mkuu wa Canada alikumbusha kuwa nchi wanachama wa G20 zinajumuisha jumla ya asilimia 75 ya idadi ya watu duniani, sehemu mbili za tatu ya Pato la Taifa la Dunia (GDP) na asilimia 75 ya biashara ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Mark Carney, Waziri Mkuu wa Canada, amesema kuwa dunia inaweza kufikia makubaliano katika masuala muhimu na kuendelea kusonga mbele hata bila uwepo wa Marekani.

Carney alitoa kauli hii baada ya kumalizika kwa mafanikio kikao cha viongozi wa kundi la G20 kilichofanyika Johannesburg. Alisema kuwa mkutano wa mwaka huu wa G20 uliokuwa wa kwanza kufanyika bila ushiriki wa Marekani, umeonyesha wazi kuwa dunia inaweza kuendelea “ikiwa peke yake.”

Akimrejea maamuzi yaliyofikiwa katika mkutano huo, Carney alisisitiza: “Makubaliano yaliyopatikana Johannesburg, licha ya vikwazo vya Washington, yana umuhimu mkubwa na yanaonesha kuwa kituo cha uzito wa uchumi wa dunia kinabadilika.”

Kwa mujibu wa Bloomberg, Waziri Mkuu wa Canada alikumbusha kuwa nchi wanachama wa G20 zinajumuisha jumla ya asilimia 75 ya idadi ya watu duniani, sehemu mbili za tatu ya Pato la Taifa la Dunia (GDP) na asilimia 75 ya biashara ya kimataifa.

Pamoja na hayo, Carney alisema Canada iko tayari kuanzisha tena mazungumzo na Marekani “wakati utakapofaa”, lakini kwa sasa “hakuna suala la haraka” la kuhitaji majadiliano ya moja kwa moja na Rais wa Marekani. Aliongeza: “Tumejikita sana kwenye mustakabali wa Canada na kujenga ushirikiano mpya. Lakini iwapo Marekani itakuwa tayari kuanza mazungumzo ya kibiashara, basi tupo tayari kuyafuatilia.”

Mkutano wa siku mbili wa viongozi wa G20 ulianza Jumamosi (22 Novemba) huko Johannesburg, mji mkuu wa kiuchumi wa Afrika Kusini.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha