Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ripoti ya Wizara ya Afya ya Palestina kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel katika Ukanda wa Gaza. Wizara hiyo ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imesema kuwa katika saa 24 zilizopita, watu 108 wameuawa na wengine 393 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya jeshi la Israel.
Aidha, wizara imeripoti kwamba watu 5 walikufa na wengine 123 kujeruhiwa walipokuwa wakijaribu kupata msaada wa kibinadamu. Jumla ya waliokufa wakiwa wanatafuta msaada hadi sasa ni 115 na waliojeruhiwa ni 1,110.
Kwa mujibu wa ripoti, bado kuna majeruhi walioko chini ya maporomoko ya majengo au mitaani ambao hawajafikika na timu za uokoaji kutokana na ukali wa mashambulizi.
Tangu tarehe 18 Machi 2025, idadi ya waliokufa imesababisha kufikia 4,603 na waliolazwa hospitalini ni 14,186.
Jumla ya waliokufa tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel tarehe 7 Oktoba 2023 imefikia 54,880 na waliopata majeraha ni 126,227.
Israel ilizindua vita dhidi ya Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba 2023 kwa malengo mawili makuu: kuangamiza harakati za Hamas na kurejesha wafungwa wake walioko eneo hilo, lakini imeshindwa kufanikisha malengo hayo.
Mnamo tarehe 19 Januari 2025, Israel na Hamas walikubaliana kusitisha mapigano na kubadilishana wafungwa, lakini Israel imeshindwa kuendelea na mazungumzo ya awamu ya pili ya mapatano ya kusitisha mapigano na kuanza tena mashambulizi mnamo tarehe 18 Machi 2025.
Your Comment