17 Oktoba 2025 - 17:41
Waziri wa Ulinzi wa Yemen: Tuko tayari kukabiliana na uvamizi wowote unaoweza kufanywa na adui

“Mohammed Nasser al-Atifi,” Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Sana’a, akitoa pole kwa viongozi wakuu wa nchi kufuatia kuuawa kwa Mkuu wa Majeshi, alisisitiza kuwa: Tuko tayari kikamilifu katika nyanja zote za kijeshi kukabiliana na shambulio au uvamizi wowote unaoweza kutokea.

Kulingana na Shirika la Habari la Kimataifa Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, al-Atifi alisisitiza kwamba Shahidi Jenerali Mkuu Mohammad Abdulkarim al-Ghammari, aliyekuwa Rais wa Stafu Mkuu wa Vikosi vya Walinzi vya Yemen, aliuawa alipokuwa akitimiza wajibu wake wa kijihad kwa kuunga mkono suala la Palestina na kusaidia wapiganaji walioko ukanda wa Ghaza.

Aliongeza kwamba shahidi al-Ghammari alitumia muda wake wote katika njia kubwa ya kijihad na alitimiza jukumu alilopewa kwa kiwango bora na cha juu kabisa.

Jeshi la Yemen katika taarifa yake ya jioni lilitangaza kifo cha Jenerali Mkuu Mohammad Abdulkarim al-Ghammari na kutoa rambirambi kwa watu wa Yemen. Katika taarifa hiyo ilielezwa kuwa roho takatifu ya shahidi al- Ghammari imepanda mbinguni akiwa shahidi miongoni mwa safu ya mashahidi wakubwa katika njia ya Al-Quds (Yerusalemu), alipokuwa akifanya wajibu wake wa kijihad na wa kidini.

Taarifa iliongeza kuwa mapigano na adui bado hayajakoma, na kwamba utawala wa Kizayuni, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, utapata adhabu yake kwa uhalifu uliotendeka hadi kuachiliwa kwa Quds na kuangamizwa kwa utawala huo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha