Kambi
-
Walioleta Kambi za Marekani Kuzunguka Iran Leo Wanalia: Kwa Nini Iran Inatushambulia?
Kwa miaka mingi, Iran iliwaonya majirani zake wa Kiarabu kuhusu hatari ya kuruhusu Marekani kujenga kambi za kijeshi katika ardhi zao, ikisema uwepo wa majeshi ya kigeni ungeweza kuzifanya nchi hizo kuwa sehemu ya vita dhidi ya Iran. Leo, baada ya kuanza kwa mapambano, kambi hizo zimegeuka kuwa maeneo ya mashambulizi, huku watawala wa Kiarabu wakijikuta wakikabiliwa na matokeo ya maamuzi waliyoyafanya hapo awali.
-
Kambi Zilizozunguka Iran Zageuka Kuwa Ramani ya Malengo: Somo la Qur’ani Kuhusu Nguvu na Maandalizi
Watu wengi walipoona kambi nyingi za kijeshi za Marekani zikizunguka Iran, walidhani kuwa Iran haitaweza kujinasua na kwamba kambi hizo zingekuwa sababu ya kuanguka kwake. Hata hivyo, kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’ani Tukufu, nguvu, maandalizi na uwezo wa kujilinda ni miongoni mwa misingi muhimu ya kukabiliana na maadui.
-
Vyombo vya Habari vya Iran: Picha za Satelaiti Zathibitisha Uharibifu wa Hangar ya Ndege za Kivita katika Kambi ya Muwafaq Al-Salti Jordan
Vyombo vya Habari vya Iran vimeripoti kuwa picha za satelaiti zinaonyesha shambulizi la usahihi lililosababisha kuharibiwa kwa hangar ya ndege za kivita katika Kambi ya Muwafaq Al-Salti nchini Jordan, ambako kuna wanajeshi wa Marekani.
-
Kwa Nini Iran Ililenga Kambi ya Al-Tanf? Ujumbe wa Kisiasa Unaozidi Ewanja wa Vita
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) wameripotiwa kulenga kambi ya kijeshi ya Marekani ya Al-Tanf, kusini mwa Syria, katika awamu ya 11 ya operesheni ya “Nasr 2”, huku wachambuzi wakisema umuhimu wa shambulizi hilo unaweza kuwa mkubwa zaidi katika ujumbe wake wa kisiasa na kimkakati kuliko matokeo yake ya moja kwa moja ya kijeshi.
-
IRGC yadai kushambulia vituo vya kimkakati vya Marekani nchini Jordan kwa makombora ya balestiki
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuwa katika awamu ya tatu ya wimbi la pili la Operesheni "Nasr-2" lililenga vituo vya kimkakati na maeneo ya wanajeshi wa Marekani katika kambi ya anga nchini Jordan kwa kutumia makombora ya balestiki.
-
IRGC yatangaza awamu ya pili ya Operesheni "Nasr 2"; yadokeza kushambulia vituo vya mawasiliano na makazi ya wanajeshi wa Marekani Bahrain
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuwa katika awamu ya pili ya Operesheni "Nasr 2" lililenga maghala ya silaha, kituo cha mawasiliano ya satelaiti na jengo la makazi ya wanajeshi wa Marekani katika Kambi ya Al-Juffair nchini Bahrain.
-
Siku Tano Zasalia kwa Kuaga Mwili wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Shahidi, Imam Sayyid Ali Khamenei
Kamati ya maandalizi ya mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Shahidi, Imam Sayyid Ali Khamenei (q.s), imetangaza kuwa zimebaki siku tano pekee kabla ya kufanyika kwa hafla ya mwisho ya kuuaga mwili wa kiongozi huyo, aliyesimama kidete kupinga mfumo wa dhulma wa kikanda kwa msaada wa Muqawama.
-
Msemaji wa Jeshi la Iran: Vita vya Siku 40 Vilidhihirisha Umoja wa Kambi ya Muqawama na Nguvu ya Kitaifa ya Iran
Msemaji wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Mohammad Akrami-Nia, amesema kuwa vita vya siku 40 vilivyoitwa "Vita vya Ramadhani" vilionyesha mshikamano wa Kambi ya Muqawama, kuimarisha uwezo wa kijeshi wa Iran na kuthibitisha nafasi ya nchi hiyo katika mlinganyo wa usalama wa kikanda.
-
IRGC Yatangaza Mashambulizi Makali zaidi ya Makombora na Ndege zisizo na Rubani Kujibu Uchokozi wa Marekani
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limetangaza kuanzisha operesheni za makombora na ndege zisizo na rubani kujibu kile lilichokiita uchokozi wa Marekani, huku likionya kuwa litachukua hatua kali zaidi dhidi ya meli zitakazokiuka maelekezo yake.
-
Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa Yatangaza Kushambulia Kambi za Marekani Kufuatia Uchokozi Dhidi ya Iran
Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa (s) yamesema vikosi vya Jeshi la Iran na Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu vimeshambulia baadhi ya kambi za Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, vikieleza kuwa hatua hiyo ni jibu kwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo ya kusini mwa Iran.
-
Kamanda Iran: Tulishambulia Kambi 17 za Marekani na Kufanya Zaidi ya Operesheni 100 Kijeshi
Kamanda wa Ulinzi wa Anga wa Jeshi la Iran kaskazini mwa nchi amedai kuwa Iran ililenga kambi 17 za kijeshi za Marekani katika eneo la kikanda na kufanya zaidi ya operesheni 100 za kijeshi zilizofanikiwa, akisisitiza kuwa mashambulizi hayo yalikuwa sehemu ya “vita vya kikanda” na kwamba mipango ya Marekani na Israel ya kuidhoofisha Iran ilishindwa.
-
Donald Trump: Iran Tayari Ina Makombora Yanayotishia Ulaya na Hivi Karibuni Kufika Marekani
Donald Trump amesema katika hotuba yake ya Hali ya Taifa kuwa Iran tayari imeendeleza makombora yanayoweza kuitishia Ulaya na kambi za kijeshi za Marekani zilizo nje ya mipaka yake, huku akidai kuwa Tehran inaendelea na juhudi za kutengeneza makombora yatakayoweza kufika hadi Marekani katika siku zijazo.
-
Leo Katika Historia:Iran Ilishambulia Kambi ya Ain al-Asad ya Marekani kwa Makombora ya Balistiki Ikiwa Kisasi cha Kuuawa kwa Jenerali Qasim Soleimani
Ilikuwa Januari 8, 2020 pindi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilipofanya Shambulizi kubwa la Kihistoria kwa kuitwanga Kambi ya Kijeshi ya Marekani iliyoitwa "Ain al-Asad" ikiwa ni sehemu ya kulipiza kiasi baada ya Kuuawa kwa Shahidi Qassem Soleimani
-
Kiongozi Mkuu wa Wahouthi: Hatutakubali Israel kutumia ardhi ya Somalia kama kambi ya kijeshi
Ikumbukwe kuwa, moja ya sababu kuu zinazotajwa katika hatua ya Israel kuitambua Somaliland ni nafasi ya kijiografia ya eneo hilo, ambayo inaonekana kuwa na umuhimu wa kimkakati kwa Israel katika kuendesha mashambulizi dhidi ya Wahouthi wa Yemen.
-
Urusi Inapanga Kuanzisha Kambi 9 za Kijeshi Katika Eneo la Kusini mwa Syria
Urusi, kwa lengo la kurejesha ushawishi wake wa kijeshi hadi mpaka wa kusini mwa Syria, inapanga kuanzisha vituo 9 vipya vya kijeshi katika mikoa ya Quneitra na Daraa.
-
Beirut - Lebanon:
Jumuiya ya Wapiga Kambi 70,000 wa Imam Mahdi (A.J) Washiriki Mkutano Mkubwa Beirut, Wakiwakumbuka Mashujaa na Kusherehekea Miaka 40 ya Jumuiya Hiyo
Sherehe hii kubwa ilifanyika kwa kaulimbiu: “Inna alal-Ahd Ya Nasrallah”, ikionyesha umuhimu wa umoja na nguvu ya kizazi kipya cha Hezbollah Lebanon.
-
Ufichuzi wa uvamizi mkubwa zaidi wa Jeshi la Israel ndani ya ardhi ya Syria tangu kuanguka kwa Serikali ya Bashar al-Assad
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa Israel wamedhibiti ukanda wa kilomita 10 kuanzia eneo la Golan hadi Hamat Ghadeer, na kuanzisha kambi mpya 8 za kijeshi katika eneo hilo.
-
Jeshi la Lebanon limepokea silaha nzito kutoka kwenye kambi za Wakpalestina
Jeshi la Lebanon limeanza mchakato wa kupokea silaha kutoka kwenye Kambi za Wapalestina katika Mji wa Sur Kusini mwa nchi hiyo.