17 Agosti 2025 - 00:16
"Majibu ya Iran yatakuwa makali zaidi iwapo adui atafanya kosa”

Jeshi Kuu la Iran lilibainisha kuwa katika tukio la kosa la kimahesabu kutoka kwa adui, kile kilichozuia operesheni kubwa wakati wa vita vya siku 12 vilivyopita hakitarudiwa tena.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jeshi Kuu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetangaza kuwa kipindi cha subira kimefikia kikomo, na Iran ipo tayari kukabiliana mara moja na kila hatua ya uadui.

Katika taarifa iliyotolewa leo (Jumamosi), Jeshi Kuu la Iran limeonya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya njama au vitisho vyovyote, na kusisitiza kuwa Iran iko tayari kujibu bila kusita tishio lolote.

Katika sehemu ya taarifa hiyo ilielezwa:
Acheni njama na tuhuma dhidi ya Iran yenye nguvu na isiyoshindwa.”

Aidha, Jeshi Kuu la Iran lilibainisha kuwa katika tukio la kosa la kimahesabu kutoka kwa adui, kile kilichozuia operesheni kubwa wakati wa vita vya siku 12 vilivyopita hakitarudiwa tena.

Taarifa hiyo iliendelea kusisitiza kuwa: “Iwapo hali kama ile ya nyuma itajitokeza, jibu la Iran litakuwa na mshangao na hatua mpya ambazo zitakuwa kali zaidi na za uharibifu mkubwa kuliko zilizopita.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha