njama
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Kumtambua Imam Khomeini ni Taa ya Kuongoza Mustakabali wa Iran
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei, amesema kuwa kuelewa na kumtambua Ruhollah Khomeini ni mwanga unaoongoza mustakabali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amebainisha kuwa kufuata mwenendo wa Ali ibn Abi Talib kumekuwa alama ya fahari kwa viongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, huku akisisitiza kwamba taifa la Iran limesimama bega kwa bega na Muqawama na kuwa mfano wa kujivunia kwa mataifa yanayotafuta uhuru. Aidha, amewataka wananchi kudumisha umoja, busara na kuaminiana ili kuvuruga njama za maadui na kulinda mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Ayatollah Mojtaba Khamenei Aonya Dhidi ya Njama za Kusababisha Mgawanyiko wa Kijamii Iran
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza umuhimu wa kulinda umoja wa wananchi, akionya kuwa adui anatumia mbinu za kueneza mifarakano ya kijamii baada ya kushindwa kufikia malengo yake kupitia mashinikizo ya kijeshi, kiuchumi na kisiasa.
-
Kiongozi jasiri na taifa imara la Iran vitashinda njama za Marekani
Hassan Fadlallah, mwakilishi wa Hezbollah katika Bunge la Lebanon, amesema kuwa kiongozi jasiri na taifa imara la Iran watafanikiwa kushinda njama za Marekani. Amesisitiza pia kuwa uchaguzi wa Bunge la Lebanon utafanyika kwa wakati wake wa kisheria bila kuahirishwa, na kwamba juhudi zozote za nje za kuingilia mchakato huo hazitafanikiwa.
-
Baghdad yafuatilia kuongezeka kwa uwepo wa ISIS
Wasiwasi wa kiusalama nchini Iraq kuhusu shughuli za ISIS mpakani na Syria umeongezeka, licha ya hatua kali za kiusalama, huku kukiwa na maonyo ya kiintelijensia na ongezeko la tahadhari.
-
Jeshi la Iran:
"Majibu ya Iran yatakuwa makali zaidi iwapo adui atafanya kosa”
Jeshi Kuu la Iran lilibainisha kuwa katika tukio la kosa la kimahesabu kutoka kwa adui, kile kilichozuia operesheni kubwa wakati wa vita vya siku 12 vilivyopita hakitarudiwa tena.
-
Mwanamke Mmoja akamatwa kwa tuhuma za kujaribu kumuua Netanyahu
Duru za Israel zimeripoti kukamatwa kwa Mwanamke mmoja kwa tuhuma za kujaribu kumuua Waziri Mkuu wa utawala huo haram wa kizayuni.