Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) -ABNA-, Vyombo vya Habari vya Israel vilidai kuwa Shin Bet ilimkamata Mwanamke Mzee katikati ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (ya Palestina) kwa tuhuma za kujaribu na kupanga kumuua Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Kulingana na vyombo vya habari vya Israel, Mwanamke huyo alinuia kumlenga Netanyahu kwa bomu.
Wakati huo huo, Polisi wa Israel pia walidai: "Kwa ushirikiano wa Shin Bet, tulimkamata Mwanamke ambaye, kwa kushirikiana na wengine, alikuwa akitaka kumuua Waziri Mkuu. Mwanamke huyu ni mkaazi wa Israel ya kati na alikuwa akitaka kumlenga Netanyahu kwa bomu."
Polisi wa Israel walisema Mwanamke huyo anachunguzwa na anakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kutekeleza kitendo cha kigaidi.
Hakuna maelezo ya kina zaidi ambayo yametolewa mpaka sasa.
Your Comment