Harakati ya Hamas imesisitiza kuwa: Mwenge wa “Dhoruba ya Al-Aqsa” utaendelea kuwaka daima, ukiwapulizia roho ya kusimamia haki, misingi, na umoja wa kitaifa. Moto wake katika nyoyo za taifa letu kubwa hautazimika kamwe, ijapokuwa kujitolea ni kwa gharama kubwa na nguvu za adui ni nyingi.
Shirika la televisheni la Kizayuni Channel 12 limekiri kwamba: “Hamas, katika kipindi cha miaka miwili migumu sana ikiwemo vita ya hivi karibuni, imeonyesha ujasiri na haijashindwa. Lengo kuu la Israel katika vita - yaani ‘kuishinda Hamas’ - halijafanikiwa.”