Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Ali Larijani ameteuliwa rasmi kuwa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran kwa amri ya Masoud Pezeshkian, Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Uteuzi huu unakuja katika kipindi cha mabadiliko ya uongozi nchini Iran baada ya uchaguzi wa hivi karibuni, ambapo Pezeshkian alichaguliwa kuwa Rais, na sasa ameanza kuweka safu ya viongozi wake katika taasisi muhimu za usalama na siasa.
Ali Larijani ni Mwanasiasa Mkongwe, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Spika wa Bunge la Iran, Mkuu wa Shirika la Utangazaji, na pia ni mmoja wa watu waliowahi kushiriki katika majadiliano ya nyuklia kwa niaba ya Iran.
Uteuzi wake katika nafasi hii nyeti unaashiria uwezekano wa mwelekeo mpya katika sera za usalama na uhusiano wa kimataifa wa Iran.
Your Comment