Ujumbe huu unaotolewa katika mnasaba wa kumbukumbu ya Shahidi Ali Khamenei unasema hivi kuwa "Ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu ndiyo msingi wa kudumu kwa matendo mema", huku ukisisitiza kwamba athari ya kweli huzaliwa na nia safi ya kumtumikia Allah (swt).
Katika hafla iliyofanyika katika shule ya wasichana ya Kigamboni, washindi wa mashindano ya kuandika muhtasari kuhusu “Shahada ya Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (ra)” walikabidhiwa zawadi maalum katika mwendelezo wa masomo ya Qur’an chini ya usimamizi wa Bi. Fatma Ma‘suma, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha elimu, ubunifu na ushindani wenye tija kwa wanafunzi.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu watu hawa Wema kwa rehema Zake zisizo na kikomo, na awajaalie makazi yao pamoja na Mtume Muhammad (rehema na amani zimshukie yeye) na Ahlul-Bayt wake watukufu na watoharifu (as).