12 Septemba 2025 - 12:06
Kuanzia Kusisitiza Umoja hadi Umuhimu wa Vyombo vya Habari na Haja ya Kuielezea Kwa Usahihi Itikadi ya Maktaba ya Ahlul-Bayt (a.s)

Katika kukaribia maadhimisho ya miaka 1500 ya kuzaliwa kwa heshima Mtume Mtukufu Muhammad (rehema na amani zimshukie yeye na Ahlul-Bayt wake) na kuzaliwa kwa furaha kwa mtoto wake mtukufu, Imam Ja'far Sadiq (amani iwe juu yake), kikao cha 195 cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kilifanyika tarehe 15/06/1404 (kwa kalenda ya Hijria Shamsia) katika mji wa Tehran, kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wajumbe wa Baraza Kuu.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) lilitoa taarifa ya mwisho baada ya kumalizika kwa kikao chake cha 195. Ifuatayo ni matini ya taarifa hiyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

"Ewe Nabii! Hakika Tumekutuma uwe Shahidi, Mbashiri na Mwonyaji (45), na mwito kwa Mwenyezi Mungu kwa idhini Yake, na taa yenye kuangaza (46). Na wabashirie Waumini kuwa wana fadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu." (Surat al-Ahzab: 45-47).

Katika kuadhimisha miaka 1500 ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w) na kuzaliwa kwa mwanawe mkubwa Imam Ja'far Sadiq (a.s), kikao cha 195 cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kilifanyika tarehe 15/06/1404 H.Sh. katika jiji la Tehran kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wanachama wa Baraza hilo.

Kikao hiki kilifanyika katika hali ambayo ulimwengu wa Kiislamu unashuhudia kuongezeka kwa njama za mabeberu wa kimataifa na utawala wa Kizayuni dhidi ya mataifa ya Kiislamu katika eneo hili, hususan Palestina, Lebanon, Iran na Yemen. Uhalifu wa kinyama wa utawala wa Kizayuni katika vita na mashambulizi yao dhidi ya raia wasio na hatia, mauaji ya raia na mashujaa pamoja na wanasayansi wa mataifa haya ni sehemu tu ya ukatili huo.

Katika kikao hiki, hali ya sasa ya kisiasa, kitamaduni na kijamii ya ulimwengu wa Kiislamu, hususan wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s) duniani kote ilijadiliwa kwa kina. Pia, masuala mbalimbali ya Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) yalishughulikiwa, na mwishoni wajumbe wa Baraza Kuu walitangaza misimamo yao kama ifuatavyo:

1. Kuhusu Umoja wa Kiislamu

Katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), washiriki wanawashauri vikali wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s) na Waislamu wote kufuata mafunzo ya Qur'ani Tukufu na Sunna Safi ya Mtume, kwa kuchukua hatua za dhati kuelekea kuimarisha umoja wa Kiislamu, kukabiliana na ubaguzi wa kikabila na tofauti za kimadhehebu, na kupinga njama za maadui za kuleta migawanyiko na udhaifu miongoni mwa Waislamu.

2. Kuhusu Arubaini ya Imam Hussein (a.s)

Tukio kubwa la kila mwaka la Arubaini ya Imam Hussein (a.s) na matembezi ya mamilioni ya wapenda Ahlul-Bayt kutoka pande zote za dunia kwenda kumzuru Imam Hussein (a.s) ni kongamano kubwa la kimataifa. Baraza Kuu linatoa shukrani za dhati kwa wananchi na serikali ya Iraq kwa kuratibu matembezi hayo, kuweka usalama, na kuwakaribisha mahujaji, na linasisitiza umuhimu wa kutumia ipasavyo fursa hii na kuchukua tahadhari dhidi ya vitisho vya maadui.

3. Kuhusu Palestina na Jinai za Israel

Katika maadhimisho ya mwaka wa pili wa jinai mpya za utawala wa Kizayuni huko Gaza na Palestina kwa ujumla, na kwa kuzingatia kimya cha jamii ya kimataifa na baadhi ya tawala za Kiarabu na Kiislamu, washiriki wanaamini kuwa njia pekee ya kukomesha mateso ya watu wa eneo hili ni kwa kuungana kwa Waislamu na wapenda haki duniani dhidi ya utawala huo. Wanasema kwamba kwa rasilimali walizonazo, Waislamu wana uwezo wa kukomesha uhalifu huu na kuikomboa ardhi ya Palestina.

Wameshutumu mipango ya upanuzi wa Israel na kuanzisha "Israeli Kubwa" na wametaka mataifa ya Kiislamu yapinge mpango hatari wa kusawazisha mahusiano kupitia "Mkataba wa Ibrahimu", na wachukue hatua madhubuti dhidi ya siasa za upanuzi wa utawala huo dhalimu.

4. Kuhusu Vyombo vya Habari na Mtandao

Mkutano umetambua kuwa vyombo vya habari na mitandao ni nyenzo zenye nguvu katika kusambaza ujumbe wa Uislamu na mafundisho ya Mitume na Maimamu (a.s), na ni jukwaa muhimu la kukabiliana na propaganda za maadui. Wamewataka wanahabari na watoa maudhui mtandaoni kujihusisha na "Jihadi ya Ufafanuzi (Jihad at-Tabyin)" na kueneza maadili ya Kiislamu kwa njia ya kielimu na sahihi.

5. Kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Washiriki wamesisitiza haki ya mataifa kujitawala, kuwa huru kikamilifu bila kuingiliwa na madola, na haki ya kujilinda dhidi ya uvamizi. Wamepongeza maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hasa mafanikio ya kisayansi na kijeshi yaliyodhihirika wakati wa vita vya siku 12 dhidi ya Wamarekani na Wazayuni, vita vilivyoisha kwa ushindi mkubwa kwa uongozi wa hekima wa Kiongozi Mkuu Ayatollah Khamenei na mshikamano wa wananchi wa Iran.

6. Kuhusu Yemen

Baraza Kuu limepongeza ushujaa wa watu na serikali ya Yemen katika kukabiliana na mashambulizi ya Kizayuni, hasa kwa kujibu jinai dhidi ya watu wa Gaza. Msimamo huo umeelezwa kuwa ni ishara ya uungaji mkono wa kweli kwa waliodhulumiwa na unapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine za Kiislamu.

7. Kuhusu Lebanon na Hizbullah

Washiriki wamempongeza Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sheikh Naeem Qassim, kwa msimamo wake thabiti dhidi ya njama za Marekani na washirika wake za kuiondoa silaha ya muqawama (mapambano ya Kiislamu). Pia wametambua hadhi ya mashahidi wa Lebanon, hususan Sayyid Hassan Nasrallah (Shahidi wa muqawama), mrithi wake Sayyid Hashem Safiuddin, na viongozi wengine wa mapambano.

8. Kuhusu Uongozi wa Jumuiya

Washiriki wametoa shukrani kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kwa kumteua tena Ayatollah Ramadhani kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), na wametambua juhudi kubwa na uongozi wa hekima wa Katibu Mkuu pamoja na wakuu wa vitengo vyote vya taasisi hii. Pia wamemshukuru wananchi wa Iran na serikali ya Jamhuri ya Kiislamu chini ya uongozi wa Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei kwa kuwa mwenyeji wa kikao hiki muhimu.

Na Mwisho wa Dua yetu ni: Alhamdulillahi Rabbil 'Alamin - Tarehe: 16/06/1404 H.Sh | 14 Rabi' al-Awwal 1447 H.Q

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha