Waumini wa Kikristo na wanajamii walioshiriki katika hafla hiyo wamepongeza hatua hiyo, wakieleza kuwa ni mfano bora wa kuishi pamoja kwa amani na kuimarisha uhusiano mwema kati ya jamii za kidini nchini Tanzania.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mkurugenzi wa Taasisi ya Khatamul Anbiyaa - Arusha, Alhaj Ghulamhussein, ameungana na waumini wa Kikristo nchini Tanzania katika kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi, kwa kufanya matendo ya kivitendo ya kijamii yanayolenga kudumisha amani, mshikamano na utu wa kibinadamu.

Katika kuenzi maana halisi ya sikukuu hiyo, taasisi hiyo imetoa msaada wa maji safi kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama, hatua inayolenga kuboresha maisha ya jamii hususan katika maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji. Aidha, taasisi hiyo pia imetoa vifaa mbalimbali kwa watoto, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwaletea faraja, furaha na matumaini katika kipindi cha sikukuu.

Akizungumza katika tukio hilo, Alhaj Ghulamhussein alisisitiza kuwa lengo kuu la msaada huo ni kuimarisha mshikamano wa kidini, kudumisha amani ya kitaifa, na kuendeleza maadili ya upendo, huruma na utu miongoni mwa Watanzania bila kujali tofauti za dini au imani. Alibainisha kuwa kuishi kwa kuheshimiana na kusaidiana ni nguzo muhimu ya kulinda amani na umoja wa nchi.

Waumini wa Kikristo na wanajamii walioshiriki katika hafla hiyo wamepongeza hatua hiyo, wakieleza kuwa ni mfano bora wa kuishi pamoja kwa amani na kuimarisha uhusiano mwema kati ya jamii za kidini nchini Tanzania.

Your Comment