Kura mpya ya maoni imeonyesha kuwa wapiga kura wa Marekani sasa wanawaamini zaidi chama cha Democratic katika masuala ya uchumi kuliko Republican. Wakati huo huo, mvutano katika Mlango wa Hormuz unaendelea kuongezeka kutokana na mapendekezo mapya ya Iran, huku ripoti zikieleza kuwa jeshi la Marekani lilitumia sehemu kubwa ya makombora yake ya masafa marefu katika vita dhidi ya Iran.
Wataalamu wa kijeshi wanaona kuwa teknolojia ya kuongozwa kwa Makombora yakiwa angani inafanya makombora hayo kuwa na faida kubwa kutokana na uwezo wake wa kurekebisha au kubadilisha mwelekeo kwa wakati halisi na Sahihi, jambo linaloongeza usahihi na kupunguza uwezekano wa kuruka hadi mbali bila kufikia shabaha yake.