28 Desemba 2025 - 08:56
Source: ABNA
Lavrov: Utawala wa Kyiv hauko tayari kwa mazungumzo yenye tija

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi amesema kuwa Ukraine haiko tayari kwa mazungumzo yenye tija (constructive).

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu shirika la habari la TASS, Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, ametangaza kuwa Moscow haioni dalili yoyote ya utayari wa utawala wa Volodymyr Zelensky na waungaji mkono wake wa Magharibi kuingia katika mazungumzo yenye tija.

Lavrov, katika mahojiano na shirika la habari la TASS kuhusu matokeo ya mwaka 2025, alisema: "Tunaona kuwa utawala wa Zelensky na walezi wake wa Ulaya hawako tayari kuingia katika mazungumzo yenye tija."

Aliongeza: "Utawala huu unawatisha raia kwa kufanya vitendo vya hujuma na kulenga miundombinu ya kiraia katika nchi yetu."

Your Comment

You are replying to: .
captcha