21 Julai 2025 - 14:51
Zanzibar | Rais Mwinyi Atoa Wito wa Kuendelea Kuliombea Taifa Amani

Alisema: “Kila ninapopata nafasi ya kuzungumza na Wananchi, nitaendelea kusisitiza juu ya umuhimu wa amani na utulivu kwa sababu ndiyo njia pekee ya kuhakikisha tunapata maendeleo.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuliombea Taifa Amani, hasa tunapoelekea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu, akisisitiza kuwa utulivu wa kitaifa ndio msingi wa maendeleo endelevu.

Zanzibar | Rais Mwinyi Atoa Wito wa Kuendelea Kuliombea Taifa Amani

Akizungumza (Siku ya Jumapili) wakati wa dua maalum kwa ajili ya kumuombea Marehemu Salim Turky, Dkt. Mwinyi alisema:

“Kila ninapopata nafasi ya kuzungumza na Wananchi, nitaendelea kusisitiza juu ya umuhimu wa amani na utulivu kwa sababu ndiyo njia pekee ya kuhakikisha tunapata maendeleo.”

Hafla hiyo ya dua ilifanyika katika makazi ya familia ya Marehemu Turky, yaliyopo Mpendae, Wilaya ya Mjini katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Rais Mwinyi alihimiza jamii iendelee kushikamana, kushirikiana na kuwa na moyo wa mshikamano katika kila nyanja za maisha, akisema kuwa amani na utulivu ni dhamana ya kila raia.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha